Upungufu/shida/ Tatizo

Kuna habari nyingi tofauti zinaenea  kuhusu uzuri au ubaya wa matibabu (sababu hizi  zinazotelewa ili kuboresha afya yetu).  Mara nyingi habari hizi si za kuaminika na pia watu wengi hawana uwezo wa kuuliza na kudhibitisha  ukweli au uhakika wa habari hizi  za afya.

Hali hii inawafanya  watu kufanya maamuzi yasiokuwa na msingi na ya kuleta hasara na kuumia. Ijapokuwa  mfumo wa elimu ulioko sasa unaangazia  wanafunzi kunakili habari bila kumwezesha mwanafunzi kujifunza kufikiria kwa undani.

Suluhu yetu

Mradi wa Informed Health Choices ni mradi wa kimataifa unaohusisha  wataalmu kutoka vitengo  mbali mbali. Mradi huu ulihusika kuchapisha kitabu cha mafunzo ya kuwezesha watu kufikiri na kutia mizani habari yoyote wanayopata kuhusu afya kabla ya kufanya maamzi. Hadi sasa, mradi huu umechapisha kitabu cha kufanya Maamzi cha Afya ya watoto wa shule ya msingi, na kinapania kuchaapisha vitabu  vingine vya mafunzo vyashule za upili na ya chuo kikuu.

Vitabu vya kufunza vya kiswahili

The cover and one spread, Children's Book in Kiswahili

Kitabu cha Maamuzi ya Afya: Kujifunza kufikiri kwa maakini kuhusu matibabu
Hiki ni kitabu cha watoto wa shule ya msingi (miaka 10-12). Kitabu hiki kina picha za ucheshi yenye mafunzo, mazoezi na orodha ya kumbukumbu.

Cover and one page of Teachers Guide in Kiswahili

Mwongozo wa waalimu
Kitabu hiki cha Maamuzi ya Afya kina mwongozo na mipangilio ya mafunzo ambayo itawawezesha  waalimu kukitumia kwa urahisi mno.

Cover and one spread of Exercise Book in Kiswahili

Kitabu cha mazoezi
Kitabu hiki kina mazoezi kutoka kitabu cha Maamuzi ya Afya.

Red and Blue activity cards

Kadi za mazoezi
Kadi hizi zitatumika kwenye  somo la saba kwenye kitabu cha Maamuzi ya Afya. Zoezi hili laonesha kubainisha kwa kutumia watu wachache yaweza kuwa  njia potofu kwa kufanya maamuzi ya afya.

Poster in Kiswahili

Orodha
Kitabu cha Maamuzi ya Afya ina Picha yenye habari muhimu ya afya.

Key concepts – image

Dhana kuu
Mfumo wa dhana kuu  katika kitabu cha Umaamuzi  wa Afya kimejumuisha dhana kuu na muhimu ambazo watu wanapaswa kujua ili kufanya maamuzi ya msingi kuhusu afya.

Vitendo endelezi

Tafsiri ya Vitabu vya walimu na wanafunzi kwa lugha ya Kiswahili ilipomalizika, vilichapishwa na vilitumika kuendeleza mafunzo  na imehusisha waalimu na shule nyingi nyingine.

Mhusika mkuu

Margaret Kaseje, Tropical Institute of Community Health & Development, Kenya

___

Please contact us if you would like high resolution files for printing.

___

IHC learning resources are in the The eGranary Digital Library, an off-line information store that provides instant access to over 35 million digital resources for those lacking adequate Internet connections.