Kuna habari nyingi tofauti zinaenea kuhusu uzuri au ubaya wa matibabu (sababu hizi zinazotelewa ili kuboresha afya yetu). Mara nyingi habari hizi si za kuaminika na pia watu wengi hawana uwezo wa kuuliza na kudhibitisha ukweli au uhakika wa habari hizi za afya.
Hali hii inawafanya watu kufanya maamuzi yasiokuwa na msingi na ya kuleta hasara na kuumia. Ijapokuwa mfumo wa elimu ulioko sasa unaangazia wanafunzi kunakili habari bila kumwezesha mwanafunzi kujifunza kufikiria kwa undani.
Mradi wa Informed Health Choices ni mradi wa kimataifa unaohusisha wataalmu kutoka vitengo mbali mbali. Mradi huu ulihusika kuchapisha kitabu cha mafunzo ya kuwezesha watu kufikiri na kutia mizani habari yoyote wanayopata kuhusu afya kabla ya kufanya maamzi. Hadi sasa, mradi huu umechapisha kitabu cha kufanya Maamzi cha Afya ya watoto wa shule ya msingi, na kinapania kuchaapisha vitabu vingine vya mafunzo vyashule za upili na ya chuo kikuu.
Kitabu cha Maamuzi ya Afya: Kujifunza kufikiri kwa maakini kuhusu matibabu
Hiki ni kitabu cha watoto wa shule ya msingi (miaka 10-12). Kitabu hiki kina picha za ucheshi yenye mafunzo, mazoezi na orodha ya kumbukumbu.
Kitabu hiki cha Maamuzi ya Afya kina mwongozo na mipangilio ya mafunzo ambayo itawawezesha waalimu kukitumia kwa urahisi mno.
Kitabu hiki kina mazoezi kutoka kitabu cha Maamuzi ya Afya.
Kadi hizi zitatumika kwenye somo la saba kwenye kitabu cha Maamuzi ya Afya. Zoezi hili laonesha kubainisha kwa kutumia watu wachache yaweza kuwa njia potofu kwa kufanya maamuzi ya afya.
Kitabu cha Maamuzi ya Afya ina Picha yenye habari muhimu ya afya.
Dhana kuu
Mfumo wa dhana kuu katika kitabu cha Umaamuzi wa Afya kimejumuisha dhana kuu na muhimu ambazo watu wanapaswa kujua ili kufanya maamuzi ya msingi kuhusu afya.
Tafsiri ya Vitabu vya walimu na wanafunzi kwa lugha ya Kiswahili ilipomalizika, vilichapishwa na vilitumika kuendeleza mafunzo na imehusisha waalimu na shule nyingi nyingine.
Margaret Kaseje, Tropical Institute of Community Health & Development, Kenya
___
Please contact us if you would like high resolution files for printing.
___
IHC learning resources are in the The eGranary Digital Library, an off-line information store that provides instant access to over 35 million digital resources for those lacking adequate Internet connections.
___
KISWAHILI / KENYA